Tuna furaha kulitambulisha kongamano kuu la wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania ambalo litafanyika hivi karibuni. Kongamano hili litasaidia katika kukuza na kuendeleza soko la ajira nchini na kuibua fursa nyingine mbalimbali za kiuchumi kwa kuwasaidia wanafunzi waliomaliza vyuo na vijana wengine ambao ni nguvu kazi ya taifa. Kongamano hili limeandaliwa kuwa jukwaa rasmi la kileo ambalo linawakutanisha wanafunzi hawa na wataalamu pamoja na wakuu kutoka sekta mbalimbali za Serikali na binafsi kujadili, kutambulisha fursa za ajira, kimaendeleo na kiuchumi katika nchi yetu na kimataifa. Kuhudhuria kwako ni hatua muhimu ya kutatua changamoto, kufaidika na mengi ndani ya saa chache tu na kujenga kesho yako imara zaidi.
Wahi kujisajili ili kupata dondoo muhimu za kongamano hadi kilele chake!
